Alhamisi 27 Novemba 2025 - 00:33
Mkuu wa Hawza Iran, Azuru Katika Ataba Tukufu

Hawza/ Mkuu wa Hawza za Kielimu Iran, kutokana na mnasaba wa kushiriki katika Kongamano la Kimataifa la Mirzai Naa’ini (r.a), alisafiri kwenda nchini Iraq.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah A‘rafi, Mkuu wa Hawza za Kielimu, alisafiri kwenda Iraq kwa ajili ya kushiriki katika Kongamano la Kimataifa la Mirzai Naa’ini (r.a).

Kwa mujibu wa taarifa hii: Sehemu ya kwanza ya Kongamano la Kimataifa la Mirzai Naa’ini ilifanyika tarehe Mosi ya mwezi wa Aban mwaka 1404 Hijria Shamsia mjini Qum, kwa ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran, na kwa ushiriki wa Ayatullah Ja‘far Subhani miongoni mwa marjaa wa taqlidi, wanazuoni, walimu na wanafunzi wa hawza za kielimu, katika Madrasa ya Kielimu ya Imamu Kazim (a.s), na katika mwendelezo wake ikafanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad.

Kongamano hili linafanyika kwa ushirikiano wa Hawza ya Kielimu ya Qum, Hawza za Kielimu ya Iraq na Ataba Takatifu, na mwendelezo wake utafanyika kwa ushiriki wa shakhsia za hawza na za kidini kutoka nchi za Kiislamu katika miji miwili ya Najafu Ashraf na Karbala, tareh sita na nane katika mwezi wa Azar shamsia.

Mirza Muhammad Hussein Gharavi Naa’ini alizaliwa tarehe 25 Dhul-Qa‘da mwaka 1276 Hijria Qamaria, sambamba na tarehe 24 Khordad mwaka 1239 Hijria Shamsia, katika mji wa Naa’in, ndani ya familia yenye elimu, katika mazingira ya kidini na nyumba iliyojaa mapenzi na huruma. Aliingia katika uwanja wa dunia, na kwa ujio wake mtukufu aliipa nyumba hiyo uchangamfu na uzuri uliokuwa zaidi.

Baba yake, Haji Mirza Abdulrahim Sheikhul-Islam, alikuwa mwanachuoni mwenye heshima na kiongozi wa kidini mwenye daraja kubwa, na babu yake alikuwa Mirza Muhammad Sa‘id Sheikhul-Islam. Mababu wake wengine pia walikuwa na wadhifa wa Sheikhul-Islam wa Naa’in, ambao ni wadhifa wa kidini uliokuwa ukitolewa kwao na sultani wa wakati wao.

Baada ya kufariki Mirza Abdulrahim, wadhifa huo ulimstahiki mwanawe mkubwa Mirza Muhammad Hussein, lakini alikataa kuupokea, na kwa hiyo ukakabidhiwa kwa ndugu yake Mirza Muhammad ‘Isa.

Familia ya Sheikhul-Islam katika mji wa Naa’in ilikuwa mashuhuri sana mbele ya watu wa kawaida na wa tabaka la juu kwa elimu na uchamungu, na ilikuwa gumzo la watu wote, na nyumba yao ilikuwa mahali pa kusuluhisha mambo na kutatua matatizo ya watu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha